OFFICIAL NEWS|| I still need help FROM WCB (Q Boy Said)|| [Watch Here]
Q Boy alifukuzwa ndani ya label hiyo baada ya kudaiwa kumruhusu shabiki kupiga picha mbele ya gai la Zari ambaye ni mama watoto wa Diamond.
Akiongea na ChafuMedia wiki hii,Q Boy amedai kuna watu wanatengeneza mazingira ili tatizo lake na WCB lionekane kubwa.
“Muziki siyo vita ujue, muziki ni kitu ambacho hauwezi kufanya bila kuomba msaada wa wadau wako wa karibu. Bado nahitaji msaada wa WCB, kesho nitakuwa na kazi ambayo nitahitaji kufanya kolabo,” alisema Q Boy.
Aliongeza, “Kwahiyo ninavyosikia watu wanazungumza vibaya kuhusu mimi na WCB najisikia vibaya kwa sababu mimi bado nahitaji msaada wao. Hata kazi zangu zilizopita wao walikuwa mstari wa mbele kunisaidia,”
OFFICIAL NEWS|| I still need help FROM WCB (Q Boy Said)||


No comments